ABIRIA KUTOKA DAR WAKWAMA NJIANI SINGIDA

ABIRIA KUTOKA DAR WAKWAMA NJIANI SINGIDA

Like
389
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

ABIRIA waliokuwa wanafanya safari kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza wamekwama njiani katika kijiji cha Chikuyu Manyoni mkoani Singida kufuatia Basi walilokuwa wakisafiria la BEST LINE kuharibika kifaa tangu majira ya Saa nane na Nusu jana Mpaka leo.

Akizungumza na Efm mmoja wa Abiria hao amesema kuwa mara baada ya kuharibika kwa gari hilo Dereva na Kondakta wamekimbia na hata walipopigiwa Simu wamedai wamekwenda Mkoani Dodoma kufuata kifaa ambacho kimeharibika na kutokurudi hadi leo.

Abiria hao wamelazimika kulala vijiji vya jirani ili kujisiriti wao na watoto na hivyo kuomba msaada wa hali na mali ili waweza kufika Mkoani Mwanza ambako ndio walikokuwa wanaelekea.

Hata hivyo EFM imeongea na Msemaji Mkuu wa SUMATRA DAVID MZIRAY ili kujua ni namna gani wanawasaidia Abiria hao na Mali zao, MZIRAY amesema kila jambo lina sheria zake hivyo amewataka Abiria hao watoe taarifa polisi huku na yeye akidai atawasiliana na SUMATRA mkoa wa Singida baadae ili kuona ni kwa jinsi gani wanatawasaidia abiria hao.

 

 

Comments are closed.