ADC YAANZA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA PENDEKEZWA KWA WANACHAMA WAKE

ADC YAANZA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA PENDEKEZWA KWA WANACHAMA WAKE

Like
246
0
Friday, 20 March 2015
Local News

CHAMA cha Alliance for Democratic Change-ADC kimeanza kukusanya maoni ya katiba pendekezwa kwa wanachama wake kote nchini ili kutoa maamuzi ya chama kwa katiba hiyo.

Akizungumza na Kituo hiki Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho DOYYO HASSAN amesema kuwa hatua hiyo inafuatia maamuzi ya mkutano mkuu wa Taifa kwa mujibu wa katiba ya chama kuwa kuwepo ushirikishwaji wa wanachama pale kunapokuwa na suala linalogusa maslahi ya Taifa.

HASSAN amesema kuwa watakwenda kukusanya maoni ya wanachama wake kote nchini katika kanda tisa za kichama na wataanzia kanda ya Dar es salaam siku ya jumapili.

Comments are closed.