AFCON: KOCHA WA IVORY COAST AMESEMA MASHINDANO YANAANZA SASA

AFCON: KOCHA WA IVORY COAST AMESEMA MASHINDANO YANAANZA SASA

Like
328
0
Thursday, 29 January 2015
Slider

Kocha wa Ivory Coast Herve Renard amesema mashindano ya kombe la mataifa Afrika yameanza sasa kwa timu yake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon siku ya jumatano ambapo ushindi huo uliwapeleka katika hatua ya robo fainali.

Kocha alisema

“kwa timu kama hii kombe la mataifa ya afrika linaanza katika robo fainali kwasababu kutolewa kabla ya kuifikia hatua hiyo ni kushindwa ” alisema kocha huyo Mfaransa ambae timu yake ameweza kupenya kwenye hatua hiyo ngumu na kuziacha timu kama Cameroon na Senegal ambazo zimeshindwa kutamba

aliongeza kwa kusema kama hautakutana na timu kama Cameroon au Ivory Coast ama Senegal basi lazima utaonyeshewa vidole

Kocha huyo amesema Mchezo kati yao na Algeria utakuwa mgumu saana kwa mara nyingine tena hivyo hapo ndipo michuano inapoanza

Comments are closed.