AFCON: MOROCCO YASHINDA BAADA YA KUKATA RUFAA

AFCON: MOROCCO YASHINDA BAADA YA KUKATA RUFAA

Like
236
0
Friday, 03 April 2015
Slider

Morocco imeshinda kesi baada ya kukata rufaa dhidi ya hukumu waliyopewa na chama cha mpira wa miguu barani Afrika Caf ambapo walifungiwa kushiriki michuano ya mataifa ya afrika Afcon kwa mwaka 2017 na 2019.

Mahakama ya usuluhishi wa mambo ya michezo imebadili maamuzi ya Caf baada ya Morocco kukosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za afcon 2015, mahakama hiyo pia imepunguza tozo iliyowekewa timu hiyo dola za kimarekani milioni moja hadi dola 50000.

Morocco amabao walipangwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo walihitaji michuano kusogezwa mbele kutokana na kuibuka kwa kasi kwa maradhi ya Ebola ila ombi hilo lilikataliwa na chama cha mpira wa miguu Afrika Caf na kufanya maamuzi ya kuhamisha michuano hiyo kwenye taifa la Equatorial Guinea

Akizungumza baada ya kushinda rufaa hiyo makamu wa rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo(FRMF) Nourredine Bouchhati amesema ni9 habari njema kwao kufuatia ushindi huo kwakumaliza tofauti zao na Caf lakini pia tayari wapo kwenye hatua za kukutana na kocha wa timu hiyo tayari kuanza ratiba mbalimbali na mazoezi

Comments are closed.