AFCON: TUNISIA YAKATA RUFAA KUPINGA KUFUNGIWA MICHUANO YA 2017

AFCON: TUNISIA YAKATA RUFAA KUPINGA KUFUNGIWA MICHUANO YA 2017

Like
308
0
Friday, 20 February 2015
Slider

Tunisia imekata rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo kufuatia kitindo cha waandaji wa michuano ya AFCON – kombe la mataifa ya Afrika kuwaondoa kwenye mashindano yatakayofanyika mwaka 2017.

Tunisia itashiriki kwenye michuano hiyo iwapo tu watakanusha madai ya rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo kufuatia kuondolewa kwao kuwa kumetawaliwa na mkanganyiko kati ya Tunisia na waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo Equatorial Guinea.

Wadie Jary alisababisha hukumu hiyo kupitishwa kufuatia kauli yake ya Mbwea hao wa jangwa hawakutendewa haki kwenye michuano hiyo baada ya mwamuzi wa mchezo raia wa Mauritia Rajindraparsad Seechurn kuwazadia ushindi wenyeji wa michuano.

Jary alitolewa kwenye mashindano pamoja na Tunisia kufungiwa kushiriki michuano hiyo mwaka 2017

Shirikisho la mpira wa miguu Tunisia (FTF) tayari wamekata rufaa na kuomba kwenda kwenye mahakama ya ngazi za juu

Comments are closed.