AFCON: VURUGU ZATAWALA MCHEZO WASIMAMISHWA DAKIKA 30

AFCON: VURUGU ZATAWALA MCHEZO WASIMAMISHWA DAKIKA 30

Like
308
0
Friday, 06 February 2015
Slider

Michuano ya kombe la mataifa ya Africa hapo jana ilichukua sura mpya katika hatua ya nusu fainali kwa kuwakutanisha wenyeji wa michuano hiyo Equatorial Guinea na Ghana.

Wachambuzi wa mpira wa miguu wamefananisha mechi hiyo na vita kufuatia vurugu kubwa zilizojitokeza uwanjani baada ya mchezo kusimamishwa kwa takribani dakika 30 baada ya fujo kuzuka kwa mashabiki wa Equitorial Guinea kuanza kurusha chupa upande wa mashabiki wa Ghana

Hali hiyo iliwalazimu polisi wa kutuliza ghasia kutumia mabomu ya machozi na helicopter uwanjani hapo ili kuweza kutuliza ghasia.

Shirikisho la mpira wa miguu la nchini Ghana liliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwa kulaumu na kuifananisha mechi hiyo na vita kufuatia mashabiki wao na wachezaji kuwa katika hali ya hatari.

tweet

Mtanange huo ulipoanzishwa mchezo ulimalizika kwa Ghana kuwa mshindi wa 3-0 ushindi utakaowapeleka faianali siku ya jumapili ambapo watakutanishwa na Ivory Coast ambayo iliicharanga DRC Congo 3-1 siku ya jumatano na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kujihakikishia kucheza fainali

Kwa upande wake raisi wa shirikisho la mpira wa miguu Kwesi Nyantakyi amesema

Afcon imekuwa michuano mikubwa na yenye mafanikio ila kwa hivi vitendo vya ubaguzi na fujo vitaaacha jeraha kwenye tasnia ya mpira wa miguu barani Afrika

_80822050_hi025741372 _80822035_hi025741727 _80822011_hi025742401 _80821976_hi025742481 _80820966_riotpolice_fans _80820964_water_riot_equatorial

Comments are closed.