AFGHANISTAN: SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA LAUA ASKARI 6 WA MAREKANI

AFGHANISTAN: SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA LAUA ASKARI 6 WA MAREKANI

Like
253
0
Tuesday, 22 December 2015
Global News

MSHAMBULIAJI wa kujitoa muhanga nchini Afghanistan amewaua askari sita wa vikosi vya Jeshi la Marekani likiwa ni miongoni mwa shambulio baya kuwahi kutokea katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Mshambuliaji huyo akiwa kwenye pikipiki, amewalenga askari wa vikosi vya muungano kati ya majeshi ya NATO na askari wa doria wa Afghanistan karibu na kambi ya vikosi vya anga.

Kamanda wa kikosi kimojawapo cha polisi amesema kwamba yeye na wasaidizi wake pamoja na kikosi cha askari walizingirwa na baadhi ya washambuliaji hali iliyowasababisha kutawanyika katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Comments are closed.