AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSEMA RAIS MUGABE NI ‘MZEE’

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSEMA RAIS MUGABE NI ‘MZEE’

Like
322
0
Friday, 11 March 2016
Global News

 

Thomson Joseph Mloyi ambae ni afisa wa polisi nchini Zimbabwe amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake kwa kusema Rais Mugabe ni mzee sana kuwa kiongozi, Afisa huyo pia anadaiwa kumtusi mke wa Rais Mugabe, Grace kuwa kahaba kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti binafsi nchini humo

 

Tuhuma dhidi yake zilianza asubuhi ya Machi 5 alipoingia katika moja ya kambi katika kambi ya Craneborne na kukuta maafisa wengine wakifanya maandalizi kwa ajili ya kazi . ndipo afisa huyo akaanza kupiga kelele kwamba “Rais Robert Mugabe ni mzee sana kutawala na kumtusi mke wake.

Mugabe aliyetimiza miaka 92 mwezi uliopita anatajwa kuwa ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani

Comments are closed.