AFISA WA KIJESHI AHAMIA KOREA KUSINI

AFISA WA KIJESHI AHAMIA KOREA KUSINI

Like
298
0
Monday, 11 April 2016
Global News

AFISA mmoja wa kijeshi wa cheo cha juu nchini Korea Kaskazini, ambaye alikuwa akisimamia masuala ya ujasusi ameihama nchi hiyo na kuelekea Korea Kusini.

Afisa huyo hajatajwa jina lakini wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini imesema kuwa alikuwa afisa wa cheo cha juu na aliondoka nchini Korea Kaskazini mwaka uliopita.

Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, limenukuu taarifa zilizosema kuwa kanali huyo alitajwa kuwa shujaa sambamba na wale walioihama Korea Kaskazini.

Comments are closed.