AFRIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA UWAJIBIKAJI NA UWAZI

AFRIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA UWAJIBIKAJI NA UWAZI

Like
188
0
Wednesday, 20 May 2015
Local News

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anafungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano  Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” unafunguliwa leo na kuhitimishwa kesho mei 21,  katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Lengo la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

Comments are closed.