AFRIKA KUSINI: 500 WAOKOLEWA NA MAGARI YA ZIMA MOTO MACHIMBONI

AFRIKA KUSINI: 500 WAOKOLEWA NA MAGARI YA ZIMA MOTO MACHIMBONI

Like
281
0
Monday, 23 February 2015
Global News

INAKADIRIWA kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini.

Moto mkubwa uliripuka mapema umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg.

Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo .

Comments are closed.