AFRIKA KUSINI: WABUNGE WATWANGANA BUNGENI

AFRIKA KUSINI: WABUNGE WATWANGANA BUNGENI

Like
358
0
Thursday, 05 May 2016
Global News

WABUNGE wa Bunge la Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni kwaajili ya kuwahutubia.

Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani.

Hata hivyo ujio wake uliwakera wabunge wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) ambao walipiga mayowe na kumtupia matusi Rais Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru wabunge hao kuondolewa nje.

Comments are closed.