AFRIKA KUSINI YAPEWA MUDA KUTOA MAELEZO YA KUSHINDWA KUMKAMATA RAIS OMAR AL BASHIR

AFRIKA KUSINI YAPEWA MUDA KUTOA MAELEZO YA KUSHINDWA KUMKAMATA RAIS OMAR AL BASHIR

Like
303
0
Friday, 16 October 2015
Global News

MAHAKAMA ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC imeipa Afrika Kusini muda zaidi kutoa maelezo ni kwanini ilishindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir anayetakiwa na mahakama hiyo kujibu mashitaka ya uhalifu wa kivita wakati alipoizuru nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu.

Nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa mkataba wa Roma, ina wajibu wa kuheshimu na kutekeleza maagizo ya mahakama ya ICC lakini serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Bashir na kumruhusu kuondoka nchini humo kinyume na agizo la mahakama.

Comments are closed.