UMOJA wa Ulaya umeahidi kutoa euro milioni 12 kama msaada kwa mataifa yanayopakana na nchi zilizoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola Afrika Magharibi.
Mali, Senegal na Ivory Coast zitanufaika na fedha hizo kuzisadia kujiandaa kukabiliana na kitisho cha mlipuko wa Ebola kupitia kampeni ya kuuhamasisha umma na kutambua mapema maambukizi.
Msaada huo mpya umetangazwa na mratibu wa juhudi za kudhibiti Ebola wa Umoja wa Ulaya Christos Stylianides kufuatia ziara yake mwezi huu katika nchi zilizoathirika sana na Ebola, Sierra Leone, Liberia na Guinea.