AFRIKA MASHARIKI HUENDA ISINUFAIKE NA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA DUNIANI KWAKUKOSA VIFAA VYA KUHIFADHIA MAFUTA

AFRIKA MASHARIKI HUENDA ISINUFAIKE NA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA DUNIANI KWAKUKOSA VIFAA VYA KUHIFADHIA MAFUTA

Like
340
0
Thursday, 12 March 2015
Local News

UTAFITI uliofanywa na kampuni ya Deloite East Africa umeonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa nchi za Afrika ya Mashariki kutofaidika na kushuka kwa bei ya mafuta duniani kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta hayo.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Kodi wa kampuni hiyo JOSPEH THOGO ambapo amesema kuwa Kushindwa kwa nchi hizo za Afrika Mashariki kuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta kunamaanisha kuwa nchi hizo zitashindwa kujikusanyia mafuta ya kutosha kwa bei nafuu kama zinavyofanya nchi nyingine.

Comments are closed.