AGIZO LATOLEWA KWA WAHANGA WA MGODI WA NYANGALATA KUFANYIWA UCHUNGUZI KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA

AGIZO LATOLEWA KWA WAHANGA WA MGODI WA NYANGALATA KUFANYIWA UCHUNGUZI KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA

Like
471
0
Monday, 07 December 2015
Local News

KATIBU MKUU wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo amewaagiza madaktari wa Hospitali ya wilaya ya Kahama kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wahanga wa Mgodi wa Nyangalata kwenda kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kwenye Hospitali za rufaa.

 

Mhandisi Chambo ameyasema hayo baada ya kuwatembelea wahanga hao waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na ajali ya kufunikwa na kifusi cha mgodi huo kwa muda wa siku 41.

 

Katibu Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia maombi yaliyotolewa na wahanga hao ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa Afya zao kutokana na kusumbuliwa na baadhi ya viashiria vinavyosababisha madhara kwenye miili yao.

Comments are closed.