AJIRA KWA VIJANA BADO NI CHANGAMOTO

AJIRA KWA VIJANA BADO NI CHANGAMOTO

Like
414
0
Thursday, 05 May 2016
Local News

MKURUGENZI wa Idara ya Ajira Ameir Ali Ameir amesema tatizo la ajira nchini bado ni changamoto kubwa kwa vijana kutokana na vijana wengi kukosa sifa za kuajiriwa na baadhi yao kuchagua kazi za kuajiriwa.

 

Ameir ameyasema hayo katika Ukumbi wa Kidongo chekundu wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wa Kamati za Ajira za Wilaya za Mjini na Magharibi.

 

Amesema vijana ndio nguvu kazi katika jamii hivyo wana nafasi kubwa katika kulitumika Taifa kwa  kufanya kazi lakini mtazamo wa vijana bado ni tatizo  na baadhi wamejenga tabia ya uvivu unaosababisha kuwepo kwa vijana wengi wanaomaliza masomo  wakiwa wazururaji wasio na ajira.

Comments are closed.