SHIRIKA lisilo la Kiserikali la AKWAYA limeanza kutekeleza mpango wa kupunguza tatizo la Utapiamlo ambalo limekithiri Wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kutoa Elimu kwa Wazazi kuweza kuwa matumizi bora ya Chakula kwa watoto.
Akizungumza na Wananchi katika Tamasha lililoandaliwa na Shirika hilo Ludewa vijijini ,Mkurugenzi wa Shirika hilo SAMWEL MPUTA amesema Wilaya ya Ludewa imejaliwa kuwa na mazao ya Chakula aina zote lakini inashangaza kuona hali ya utapamlo iko juu.
MPUTA amebainisha kuwa Mpaka sasa Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Asilimia 52 ya Watoto Waishio mkoani Njombe wana tatizo la Utapiamlo hali inayosababishwa na wazazi kushindwa kupanga Matumizi Bora ya chakula kwani muda mwingi wamekuwa wakiwaaacha watoto wajihudumie wakati wao wakishinda katika Vilabu vya Pombe.