AL SHABAAB ALIYEJIUNGA NA IS ANASWA SOMALIA

AL SHABAAB ALIYEJIUNGA NA IS ANASWA SOMALIA

Like
260
0
Monday, 25 April 2016
Global News

KAMANDA wa kundi la al-Shabaab aliyejiunga na kundi linalojiita Islamic State nchini Somalia amekamatwa na maafisa wa usalama nchini humo.

 

Hassan Mohamed Siad ambaye pia hujulikana kama Hassan Fanah alikamatwa jana Jumapili baada ya maafisa wa ujasusi wa Somalia kufanya operesheni katika nyumba moja mtaa wa Kahda.

 

Vyombo ya habari nchini Somalia vinasema alikuwa anajificha katika mtaa huo kutoka wa wapiganaji wa al-Shabab. Serikali ya Somalia ilikuwa imeahidi zawadi ya $2,000 kwa mtu ambaye angetoa habari za kusaidia kukamatwa kwake.

Comments are closed.