AL SHABAAB WAKIRI KUHUSIKA NA SHAMBULIZI MANDERA,KENYA

AL SHABAAB WAKIRI KUHUSIKA NA SHAMBULIZI MANDERA,KENYA

Like
248
0
Tuesday, 07 July 2015
Global News

WANAMGAMBO wa kundi la Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulizi lililotokea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo watu 14 wameuawa usiku wa kuamkia leo.

Taarifa za awali zimeonesha kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wengi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji katika maeneo hayo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa mashambulizi kama hayo yametishia kudumaza shughuli za maendeleo na kiuchumi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake ni watu kutoka maeneo ya nje ya nchi hiyo.

Comments are closed.