AL-SHABAB WADHIBITI MIJI ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA MAJESHI YA KENYA

AL-SHABAB WADHIBITI MIJI ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA MAJESHI YA KENYA

Like
299
0
Wednesday, 27 January 2016
Global News

WAPIGANAJI wa kundi la Al-Shabab wameingia na kudhibiti miji ambayo majeshi ya Kenya yaliondoka jana nchini Somalia.

Wakazi wa maeneo ya jirani na miji hiyo wamewaambia waandishi wa habari kwamba wapiganaji wa kundi hilo la Kiislamu wameingia kwenye miji ya Al-Adde, Hosingoh na Badhaadhe.

Katika mji wa Hosingoh, mamia ya wapiganaji wanaripotiwa kuingia na kuhutubia wakazi na kisha wakamteua kiongozi wa kusimamia eneo hilo.

Comments are closed.