GABON: VURUGU ZATANDA BAADA YA ALI BONGO KUTANGAZWA MSHINDI

GABON: VURUGU ZATANDA BAADA YA ALI BONGO KUTANGAZWA MSHINDI

Like
441
0
Thursday, 01 September 2016
Slider

_90989705_mediaitem90989704

Fujo zimezuka katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.

Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia makao makuu ya chama chake.

Serikali imesema inawaandama “wahalifu wenye silaha” ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge.

Bw Ping amepinga matokeo ya urais ambayo yalionyesha Rais Bongo alishinda uchaguzi kwa kura chache. Hii inampa fursa ya kuongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka saba.

“Walishambulia mwendo wa saa 01:00 (00:00 GMT). Ni kikosi cha wanajeshi walinzi wa rais. Walikuwa wanarusha mabomu kutoka kwa helikopta na kisha baadaye wakashambulia kutoka ardhini,” Bw Ping, ambaye hakuwa katika makao makuu hayo wakati huo, alisema awali. Ameomba usaidizi kutoka kwa jamii ya kimataifa kulinda raia

._90989387_mediaitem90989386

Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi kwa 49.8% ya kura, akifuatwa na Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura zilizowatenganisha zikiwa 5,594.

Bw Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na “hakuna ajuaye” hasa nani alishinda.

_90989383_mediaitem90989382

#BBC

Comments are closed.