alinusurika kunyongwa mara tatu

alinusurika kunyongwa mara tatu

3
1935
0
Thursday, 21 February 2019
Global News

Katika hukumu ya kifo nchini Malawi,Byson Kaula alikuwa karibu anyongwe mara tatu lakini kila zamu yake ilipofika, mnyogaji aliacha kunyonga na kudai kuwa amechoka kabla hajamaliza watu wote ambao waliokuwa kwenye orodha yake.

Hivyo kutokana na kuhairishwa huko Kaula aliweza kunusurika kifo mpaka taifa hilo lilipoacha kutoa adhabu ya kunyonga.

Byson Kaula anasema kuwa ni jirani zake wenye wivu ndio walihusika kusababisha yeye apatikane na hatia ya uuaji.

Ilikuwa mwaka 1992, wakati aambapo mtu akiua hukumu ya kunyongwa ilikuwa ni lazima.

Byson alikulia katika kijiji kidogo kusini mwa Malawi na baadae aliweza kupata kipato akilichomtosha kwa kufanya kazi katika kiwanda cha gesi kilichopo Johannesburg, Afrika kusini.

Na aliporudi nyumbani aliweza kununua ardhi na kuajiriwi watu watato ambao walikuwa wanamlimia mazao ya chakula na matunda.

“Niliporudi nyumbani baada ya mafanikio ndio wakati wa huzuni ulipoanza,”Byson alisema.

Majirani walimvamia mmoja wa wafanyakazi wangu na kumuacha akiwa amejeruhiwa, Byson alisema.

Mwanaume huyo alivyoumizwa alishindwa kutembea bila msaada na wakati alipoenda kumsaidia kwenda maliwatoni, kwa bahati mbaya alianguka chooni.

Mwanaume huyo alikufa mara baada ya kufikishwa hospitalini, na wakati huo Byson alikuwa na umri wa miaka 40 alishitakiwa kwa mauaji.

Majirani zake Byson walitoa ushaidi dhidi yake mahakamani.

Mama yake aitwaye Lucy hakusikia kile ambacho kilikuwa kinaendelea mahakamani kwa sababu alikuwa amekaa nyuma na alipouliza nini kilichoendelea aliambwa kuwa mwanae amehukumiwa kunyongwa, machozi yalimmiminika tu mpaka kifuani.

Kipindi hicho kilikuwa wakati wa utawala wa serikali ya Banda, mwaka 1964.

Byson anakumbuka vyema mateso yote ambayo aliyapitia wakati anasubiri kunyongwa kwa mashine.

“Nilipoambiwa kuwa ninaweza kwenda niko huru na muda wangu wa kusubiri kunyongwa umeisha’ -yani nilijihisi kwanza kuwa nilishakufa tayari.”

Byson anakumbuka siku moja aliambiwa kuwa jina lake lipo kati ya watu 21 ambao watanyongwa ndani ya saa chache. Walinzi walimwambia kuwa awe tayari kunyongwa majira ya saa saba, hivyo inabidi asali maombi yake ya mwisho.


Watu waliendelea kunyongwa mpaka saa tisa, ndipo mnyongaji akaacha kufanya kazi hiyo wakati alikuwa hajamaliza watu ambao alikuwa nao katika orodha.

Watu watatu walinusurika, Byson akiwemo katika majina hayo.

“Alikuwa mtu mmoja tu ndio anaiendesha mashine hiyo. Na siku hiyo nilielewa kuwa alikuwa amechoka na alikuwa anatokea Afrika kusini, hivyo alivyoghairi alidai kurudi tena mwezi ujao”,Byson alisema.


Jambo hilohilo la mnyongaji kuchoka kabla hajamaliza orodha yake lilijirudia mara mbili zaidi na Byson akaachwa hai.

Kuna wakati ambapo wengine wote waliohukumiwa kunyongwa walinyongwa bali alibaki yeye tu”. Byson alisema.

Kwa namna ambavyo alikuwa na bahati ya kupona kunyongwa, yeye mwenyewe alijaribu kujiua mara mbili na kupona pia.

Baada ya vyama vingi kuanzishwa nchini Malawi mwaka 1994 , unyongwaji ulisitishwa na hukumu hiyo ikawa inatolewa tu pale ambapo rais atasaini lakini kwa miaka 25, hakuna rais aliyesaini ili wafungwa wanyongwe au wafungwe maisha.

Muda ulivyoendelea kusogea, Byson alipata elimu ya gerezani na kuondolewa hukumu ya kifo kuwa kifungo cha maisha.

Mwaka 2007, karibu nusu karne tangu Byson afungwe, kesi moja ya kihistoria ilibadili kila kitu.

Mtumia madawa ya kulevya ambaye alikiri kumuua mama yake wa kambo, lakini alidaiwa kuwa hana akili vizuri alipoenda mahakamani na kuhoji juu ya hukumu ya kifo.Alitaka hukumu hiyo iangaliwe vizuri katika katiba ya nchi hiyo ili hukumu hiyo iweze kutolewa kwa haki.

Na mara baada ya hukumu za kifo za wafungwa 170 kuhakikiwa, wafungwa 139 waliachiwa huru.

Ingawa kwa mujibu wa kituo cha sheria cha kujitolea alidai kuwa wengi walioachiwa huru walipatwa na matatizo ya akili na wengine walipata ulimavu.

Zaidi ya nusu ya wafungwa waliachiwa huru walikuwa hawamo hata kwenye rekodi ya mahakama, na wengine ilikuwa haieleweki kwa nini walikuwa geezani.

“Ilikuwa kama ninaota -sikuamini kile ambacho jaji alikisema” Byson alisema.

Byson aliachiwa huru aliwa na miaka 60, na sasa anajitolea kwenda gerezani mwishoni mwa wiki ili kutoa ushauri kwa wafungwa kwa kueleza kile alichopitia.

Mke wake alifariki dunia wakati yeye yuko gerezani na kuwaacha watoto sita ambao aliwakuta wamekuwa tayari baada ya kukaa muda mrefu gerezani.

Byson anaishi mwenyewe ila anamtunza mama yake ambaye ana umri wa miaka 80.

Hukumu ya kifo imesalia kuwa ni ya lazima kwa baadhi ya visa vya uhalifu – na kubaki kuwa miongoni mwa hukumu yenye utata duniani.

Kwa sehemu kubwa, imekuwa ikipingwa mahakamani, huku baadhi ya nchi ikiiondoa katika katiba yake, baada ya kugundua inakinzana na haki za binadamu.

 

cc: BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *