ALSHABAAB YASHAMBULIA KAMBI YA AMISOM

ALSHABAAB YASHAMBULIA KAMBI YA AMISOM

Like
197
0
Tuesday, 01 September 2015
Global News

KUNDI la wapiganaji wa Kiislamu la Al – Shabaab limeshambulia kambi ya kikosi cha walinda usalama wa muungano wa Afrika AMISOM na Kujeruhi watu wengi katika shambulio hilo.

Al-Shabaab wamejisifia kuwa mmoja wa walipuajI wake wa kujitolea ameliendesha gari liliolkuwa na bomu ndani ya kambi ya Janale umbali wa kilomita 90 kutoka mji mkuu Mogadishu kisha wapiganaji wake wengine wakashambulia kwa risasi.

Kwa mujibu wa Al shabaab, wanajeshi hamsini wa AMISOM wameuawa japo ripoti hizo hazijathibitishwa kutoka upande wa AMISOM.

AL2

Jengo lililoshambuliwa na Al shabaab mjini Mogadishu

Comments are closed.