AMNESTY INTERNATIONAL YATUHUMU MUUNGANO UNAOONGOZWA NA SAUDI ARABIA

AMNESTY INTERNATIONAL YATUHUMU MUUNGANO UNAOONGOZWA NA SAUDI ARABIA

Like
218
0
Friday, 11 December 2015
Global News

SHIRIKA  la  kutetea  haki  za  binadamu la  Amnesty International limesema  jana  kuwa  muungano unaoongozwa  na  Saudi  Arabia umeshambulia  kwa mabomu shule  nchini  Yemen, na  kukiuka sheria  za kimataifa  za  kiutu na kuzuwia  maelfu  ya  watoto  kupata elimu.

 

Shirika  hilo  lenye makao  yake  makuu  mjini  London limeyataka  mataifa  yote  ambayo  yanaupatia  silaha muungano wa  kijeshi  unaoongozwa  na  Saudi Arabia , ikiwa ni  pamoja  na  Marekani na  Uingereza, kusitisha  upelekaji wa  silaha  ambazo  zinatumika  katika  ukiukaji  huo wa sheria  za  kimataifa.

 

Comments are closed.