AMNESTY YATAKA KURA YA VETO ITUMIKE KUFUATIA MAUAJI YA HALAIKI

AMNESTY YATAKA KURA YA VETO ITUMIKE KUFUATIA MAUAJI YA HALAIKI

Like
362
0
Wednesday, 25 February 2015
Global News

SHIRIKA la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limetoa wito kwa Wanachama watano wa kudumu wa Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kutumia kura yao ya Veto kwa maswala yahusuyo mauaji ya halaiki.

Shirika hilo limesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiweka maslahi ya nchi mbele kuliko maswala ya haki za binaadam.

Katika Ripoti yake ya mwaka, Amnesty International imesema mwaka 2014 ulikuwa mwaka wenye matukio mabaya kwa mamilioni ya Watu waliokuwa kwenye maeneo yenye migogoro, na kusikitishwa na namna dunia ilivyoshughulikia matatizo hayo.

 

Comments are closed.