ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA MADRID OPEN

ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA MADRID OPEN

Like
298
0
Wednesday, 04 May 2016
Slider

Mwingereza Andy Murray ameanza vyema kutetea taji lake katika michuano ya Madrid Open kwa ushindi wa seti 7-6 7-3 3-6 na 6-1 dhidi ya Radek Stepanek.

Ilichukua muda wa saa mbili na dakika 16 kwa Murry kumshinda Stepanek raia wa Czech mwenye miaka 37.

”Sikucheza michezo mingi kipindi cha nyuma.Ilikua ngumu sana,”alisema Murray mwenye miaka 28 ambaye atakutana na Gilles Simon ama Pablo Busta katika mzunguko wa tatu siku ya Alhamisi.

Mapema kwenye mchezo wa awali Muhispaniola Rafael Nadal alimshinda Andrey Kuznetsov wa Urusi kwa seti 6-3,6-3.

Nadal ambaye alifungwa alipocheza na Murray katika fainali za mwaka jana anaweza kukutana tena na mpinzani wake huyo katika nusu fainali za mwaka huu.

Kinara nambari moja wa mchezo huo duniani Novak Djokovic atashuka dimbani siku ya jumatano kukipiga dhidi ya Borna Coric kutoka Crotia.

Comments are closed.