KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel anakutana leo na waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , ambaye amemlaumu kansela kwa kusisitiza kuhusu hatua ya kubana matumizi kwa nchi yake ambayo imesababisha mzozo wa kiutu wa umasikini pamoja na ukosefu mkubwa wa ajira.
Viongozi hao wa Ugiriki na Ujerumani wanakutana mjini Berlin baada ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi kuhusiana na matatizo ya upatikanaji wa fedha kwa Ugiriki , hisia za baada ya vita na ishara zinazoelekea kuwa za kauli mbaya zilizotolewa na viongozi.
Waziri wa uchumi wa Uhispania Luis de Guindos amesisitiza kuwa nchi hiyo haitapatiwa fedha hadi pale itakapotekeleza mageuzi yote yaliyopendekezwa.