ANGELA MERKEL: SULUHU YA MZOZO WA WAHAMIAJI ITAPATIKANA NJE YA ULAYA

ANGELA MERKEL: SULUHU YA MZOZO WA WAHAMIAJI ITAPATIKANA NJE YA ULAYA

Like
211
0
Friday, 20 November 2015
Global News

KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amesema mzozo wa wahamiaji unaolikumba bara la Ulaya utasuluhishwa katika mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya na mbali ya mipaka hiyo.

Akizungumza akiwa na Kansela wa Austria Werner Faymann, Merkel amesema Ulaya inahitaji uimara na kasi zaidi kuhusu kushughulikia maeneo yaliyo na utata ikiwemo Ugiriki ambako wakimbizi na wahamiaji wanaweza kusajiliwa.

Ujerumani imeshuhudia ongezeko la wahamiaji huku ikiwapokea zaidi ya wahamiaji laki saba hadi kufikia mwezi uliopita.

Comments are closed.