ANGLO GOLD ASHANTI YAJITOLEA KUWEZESHA MATIBABU YA UGONJWA WA MIDOMO SUNGURA KANDA YA ZIWA

ANGLO GOLD ASHANTI YAJITOLEA KUWEZESHA MATIBABU YA UGONJWA WA MIDOMO SUNGURA KANDA YA ZIWA

Like
319
0
Friday, 13 November 2015
Local News

KAMPUNI ya uchimbaji Madini ya Anglo Gold Ashanti imejitolea kuwezesha huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Midomo sungura Katika kanda ya ziwa matibabu yanayotarajia kufanyika katika hospitali ya Rufaa ya Sokoe Toure jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango huo Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo Tenga Tenga amesema miongoni mwa majukumu ya kampuni hiyo ni pamoja na kusaidia jamii kujikwamua na matatizo mbalimbali na kuwataka wananchi wanaosumbuliwa na ugonjwa huo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kupata huduma.

Tenga amesema Kampuni hiyo inatarajia kutoa huduma hiyo ikilenga Watanzania wote hususani wale wa kanda ya ziwa kwa kuwa ugonjwa huo umekithiri katika maeneo hayo.

Comments are closed.