ANNE MAKINDA ATANGAZA KUTOWANIA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE NA KUACHANA NA SIASA

ANNE MAKINDA ATANGAZA KUTOWANIA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE NA KUACHANA NA SIASA

Like
254
0
Friday, 13 November 2015
Local News

WAKATI viongozi mbalimbali wakijitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Anne Makinda amesema hatogombea nafasi hiyo na kwamba ameachana na masuala ya kisiasa kwa kuwa amejishughulisha na masuala hayo kwa kipindi cha miaka 40.

 

Makinda ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wake wa kuwania nafasi hiyo ambayo tayari ameshaipitia.

 

Akizungumzia namna alivyoweza kuliongoza bunge kwa kipindi alichokuwa Spika wa Bunge hilo amesema kuwa amejitahidi kuendesha shughuli zote za Bunge ingawa kulikuwa na changamoto nyingi kutoka kwa baadhi ya wabunge.

Comments are closed.