ANUSURIKA KIFO KWA KUDHANIWA NI JAMBAZI

ANUSURIKA KIFO KWA KUDHANIWA NI JAMBAZI

Like
374
0
Monday, 16 May 2016
Local News

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa kijiji cha Manyinga Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati wakiwa doria usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa upelelezi wilaya ya mvomero ASP Peter Majengo akizungumza na wananchi waliokusanyika katika hospitali hiyo amesema tukio hilo lilitokea usiku wakati askari wakiwa doria na walipomuona walimsimamisha kijana huyo na kumtilia shaka kuwa ni jambazi ndipo walimfyatulia risasi na kumjeruhi sememu ya shingo.

Comments are closed.