APC WAKOSOA KUAKHIRISHWA UCHAGUZI NIGERIA

APC WAKOSOA KUAKHIRISHWA UCHAGUZI NIGERIA

Like
247
0
Monday, 09 February 2015
Global News

UPINZANI  nchini Nigeria umekosoa hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi hadi mwishoni mwa Mwezi March.

Chama kikuu cha upinzani cha APC kimesema hatua hiyo ni kikwazo kikubwa kwa Demokrasia nchini humo. Na kwamba Jeshi la Nigeria limelazimisha kuahirishwa kwa Uchaguzi ili liweze kumsaidia Rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan kwenye Kampeni zake.

Uchaguzi mkuu nchini humo ulipangwa kufanyika jumamosi ijayo lakini Tume ya Uchaguzi imesema Mashambulizi ya Boko Haram kwa kiasi kikubwa yanahatarisha uwepo wa zoezi la uchaguzi ,Usalama wa Wapigakura, lakini pia waangalizi wa Uchaguzi.

Comments are closed.