MAELFU ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Argentine – Buenos Aires katika harakati za kupinga mateso dhidi ya mwanamke .
Maandamano hayo yamekuja kufuatia matukio ya mara kwa mara ya visa vya mauaji kwa wanawake yaliyoshtua Taifa hilo yakiwemo ya mwalimu wa chekechea kwa kukatwa koo na mumewe mbele ya darasa lake.
Vyama vya wafanyakazi kwa kushirikiana na vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo ambapo kwa sasa tayari Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa mwanamke nyumbani.