ARNOLD PERALTA APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA

ARNOLD PERALTA APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA

Like
315
0
Friday, 11 December 2015
Slider

Mchezaji wa kimataifa wa Honduras Arnold Peralta apigwa risasi na kufa wakati akiwa mapumzikoni kwenye mji wake wa nyumbani.

Mauaji hayo yametokea kwenye maegesho ya magari katika eneo la maduka huko La Ceiba kwenye ufukwe wa Caribbean ambapo chanzo cha uvamizi huo hakijawekwa wazi.

Kiungo huyo mwenye miaka 26 anaeichezea klabu ya Olimpia kwenye jiji kuu la Tegucigalpa

Taifa hili la Honduras linatajwa kuwa moja ya nchi za viwango vya juu vya makundi ya uhali duniani.

Osman Madrid mkurugenzi wa shirikisho la soka nchini humo amesema wamesikitishwa na kifo cha mchezaji huo na kutaja kuwa taifa hilo linahuzunika kumpoteza moja ya vijana wake tegemezi kabisa

Comments are closed.