ARSENAL YAAGA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

ARSENAL YAAGA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

Like
282
0
Wednesday, 18 March 2015
Slider

Arsenal imeshindwa kuifikia hatua ya robo fainali ya michuano ya Mabingwa huko barani Ulaya richa ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini katika mchezo wao wa jana usiku.

Klabu hiyo ya washika bunduki jana imeshindwa kusonga mbele kutokana na kosa la kuruhusu magoli mengi wakiwa nyumbani pale walipopokea kichapo cha 3-1 dhidi ya Monaco.

Kwa matokeo hayo klabu hiyo itaikosa hatua hiyo muhimu ya robo fainali ikiwa ni mara ya tano mfululizo

Goli la kwanza la Arsenal lilitiwa nyavuni dakika ya 36 na Olivier Giroud na kuinua mashabiki wa klabu hiyo na la pili lilifungwa na Aaron Ramsey mnamo dakika ya 79 ya mchezo.

Matokeo ya klabu zote mbili kwa ujumla ni 3-3 kwa matokeo hayo Monaco itasonga mbele kwakuwa na magoli mengi ya ugenini

Comments are closed.