ARSENAL YAILAZA  OLYMPIAKOS 3-0

ARSENAL YAILAZA OLYMPIAKOS 3-0

Like
301
0
Thursday, 10 December 2015
Slider

Olivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Gunners wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kulaza Olympiakos.

Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F.

Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell.

Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia penalti.

Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa Athens.

Takwimu muhimu:

  • Olivier Giroud ndiye mchezaji wa nne kufungia Arsenal hat-trick kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).
  • Vijana wa Arsene Wenger wameshinda mechi yao ya kwanza Ugiriki tangu Desemba 1998 (3-1 dhidi ya Panathinaikos).
  • Giroud ndiye mchezaji was aba wa Arsenal kufikisha magoli kumi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (wengine wakiwa Henry, van Persie, Ljungberg, Fabregas, Walcott na Pires the others).
  • Matokeo ya Jumatano yalifikisha kikomo msururu wa kutoshindwa wa Olympiakos wa mechi sita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu za Uingereza(Kushinda 5, Sare 1)
  • Arsenal walikuwa wameshindwa mechi tatu zao za awali ugenini dhidi ya Olympiakos zote katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, zote katika mechi ya sita hatua ya makundi.

Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano:

  • Bayer Leverkusen 1 – 1 Barcelona
  • Olympiakos 0 – 3 Arsenal
  • Chelsea 2 – 0 FC Porto
  • Valencia 0 – 2 Lyon
  • Roma 0 – 0 BATE Borisov
  • Dinamo Zagreb 0 – 2 Bayern Munich
  • Dynamo Kiev 1 – 0 M’bi Tel-Aviv
  • KAA Gent 2 – 1 Zenit St Petersburg

Comments are closed.