ARUSHA: SUMATRA YATAKIWA KUSHUGHULIKIA TATIZO LA UTOAJI WA NAULI ZISIZO IDHINISHWA

ARUSHA: SUMATRA YATAKIWA KUSHUGHULIKIA TATIZO LA UTOAJI WA NAULI ZISIZO IDHINISHWA

Like
348
0
Wednesday, 27 May 2015
Local News

WAZIRI wa Uchukuzi mheshimiwa SAMWEL SITTA ameagiza meneja wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA-mkoa wa Katavi kushughulikia haraka tatizo la utozwaji wa nauli zisizo idhinishwa na mamlaka hiyo katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Mheshimiwa SITTA ametoa agizo hilo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Nkasi mheshimiwa ALLY KESSY aliyetaka kufahamu uhalali wa nauli hizo kutoka kwa mamlaka hiyo.

Mbali na hayo waziri amesema kuwa ni muhimu kwa Sumatra katika kila eneo kuhakikisha inafuatilia kwa makini suala la utozwaji wa nauli ili kuwatendea haki  wananchi.

Comments are closed.