ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMJERUSHI MKEWE NA PANGA

ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMJERUSHI MKEWE NA PANGA

Like
316
0
Tuesday, 31 March 2015
Local News

POLISI Mkoani Katavi  inamshikilia mkazi  wa kitongoji cha Ntumba , Kijiji cha Mnyengele  Wilayani Mpanda , DEOGRATIAS PASTORI  kwa kumjeruhi  mkewe  kwa  kumkata mkono  wa kushoto  na kupasua  tumbo  la Mgoni wake  kwa panga .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , DHAHIRI KIDAVASHARI  amethibitisha  kutokea kwa tukio hilo usiku  katika kitongoji cha Ntumba kijiji cha Mnyagala  Kata ya Mnyagala  Wilayani Mpanda.

KIDAVASHARI amewataja majeruhi hao  kuwa ni  pamoja  na  Mke wa mtuhumiwa  TABU NESTORY, MASAGA ELIAS ambao  wamefumaniwa na  mtuhumiwa  wakifanya mapenzi  jikoni nyumbani kwake kijijini humo .

Comments are closed.