ASILIMIA 11.7 HAWANA AJIRA TANZANIA

ASILIMIA 11.7 HAWANA AJIRA TANZANIA

Like
343
0
Tuesday, 24 February 2015
Local News

NAIBU Waziri wa kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, amesema kuwa hali ya ukosefu wa ajira nchini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi uliofanyika mwaka 2006, jumla ya watu waliokuwa hawana kazi hapa nchini ni asilimia 11.7.

Ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa Semina ya vijana Mkoa wa Lindi, na kusema kuwa utafiti huo umeonyesha kuwa takribani asilimia 13.4 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 wa Tanzania hawana kazi kabisa.

Mheshimiwa Makongoro Mahanga, ameeleeza kuwa ukosefu huo wa ajira kwa vijana ni mkubwa zaidi asilimia 26.7 ukilinganisha na vijijini asilimia 7.9 ,ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutofikiwa kikamilifu kwa malengo ya nchi ya kuinua uchumi katika sekta za kilimo, uzalishaji na viwanda.

 

Comments are closed.