ASILIMIA 14.3% WAFAULU MITIHANI YA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU

ASILIMIA 14.3% WAFAULU MITIHANI YA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU

Like
303
0
Wednesday, 23 December 2015
Local News

JUMLA ya watahiniwa 813 ambao ni sawa na asilimia 14.3 wamefaulu mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)  uliofanyika Novemba 2015 kote nchini.

 

Katika matokeo hayo, wahitimu wengine elfu 1,867 ambao ni sawa na asilimia 32.9 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali kati ya watahiniwa elfu 6,404 waliosajiliwa katika mitihani hiyo.

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi NBAA Bwana. Pius Maneno katika kikao cha wakurugenzi wa bodi hiyo kilichokaa kuidhinisha matokeo hayo jijini Dar es salaam.

Comments are closed.