ASILIMIA 80 YA WAGONJWA WA SARATANI NCHINI HUFIKA HOSPITALI WAKIWA NA HALI MBAYA

ASILIMIA 80 YA WAGONJWA WA SARATANI NCHINI HUFIKA HOSPITALI WAKIWA NA HALI MBAYA

Like
200
0
Thursday, 08 October 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa Tanzania inapokea idadi ya wagonjwa wapya takribani elfu 44,000 kila mwaka lakini wengi wao kwasababu mbalimbali hawafiki Hospitalini, na ni asilimia 10 tu ya wagonjwa ndio wanaofika katika Taasisi ya Saratani Ocean road.

Hata hivyo kati ya hao takribani asilimia 80 hufika wakiwa katika hatua za juu za ugonjwa, hali ambayo hupunguza uwezekano wa kutoa matibabu ya kuponyesha ugonjwa wao.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dokta Diwani Msemo amesema kuwa bila michango ya wadau katika juhudi za kutokomeza ugonjwa huu wa saratani, nguvu za Serikali pekee haziwezi kufanikiwa.

Comments are closed.