ASKARI MAGEREZA KUAZIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

ASKARI MAGEREZA KUAZIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Like
406
0
Friday, 04 December 2015
Local News

KATIKA kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika Disemba 9 mwaka huu, watumishi wapatao 39 wa Jeshi la Magereza nchini wanatarajiwa kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Washiriki hao wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Minja amesema amefurahishwa na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la Magereza nje ya mipaka yake.

Comments are closed.