ASKOFU MKUU wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda leo.
Papa Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda leo kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.
Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania–TEC, Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo.