ASKOFU MKUU TABORA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE ZIARA YA PAPA FRANCIS UGANDA

ASKOFU MKUU TABORA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE ZIARA YA PAPA FRANCIS UGANDA

Like
260
0
Friday, 27 November 2015
Local News

ASKOFU MKUU wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda leo.

 

Papa Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda leo kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.

 

Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania–TEC, Padre Raymond Saba amesema  Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo.

Comments are closed.