ATLETICO MADRID YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA KWA MIKWAJU YA PENATI

ATLETICO MADRID YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA KWA MIKWAJU YA PENATI

Like
510
0
Wednesday, 18 March 2015
Slider

Atletico Madrid imetinga robo fainali za michuano ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Bayer Leverkusen kwa mikwaju ya penati.

Klabu hiyo ya nchini Hispania ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Bayer Leverkusen kutokea Ujerumani.

Hatua hiyo ya kutembezeana mikwaju ya penati ilikuja baada ya dakika 120 za mchezo huo kumalizika huku wenyeji Atletico Madrid wakiwa mbele kwa goli moja

Goli hilo moja lilishindwa kuifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi kutokana na matokeo ya mchezo wa awali ambapo Leverkusen iliitandika Atletico bao moja kwa bila.

Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za wageni wao na kutinga moja kwa moja katika hatua ya robo fainali

AT5 AT2 AT

Comments are closed.