AU: YAKUTANA DAR LEO

AU: YAKUTANA DAR LEO

Like
273
0
Thursday, 27 November 2014
Local News

UMOJA WA AFRICA na nchi zake 13 ikiwemo Tanzania zimekutana leo nchini kujadili mpango wa muda mfupi wa kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote Africa ACIRC.

 Mpango huo wa ACIRC uliounda jeshi la Afrika la kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote kupitia zoezi la utulivu, Africa imelenga kutimiza malengo ya nchi za umoja huo kwa kupima uwezo wa kutatua matatizo yake yenyewe   ambapo kwa mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla hiyo.

Akizungumza  na waandishi wa habari jijini  Dar es salaam Meja Jenerali wa Jeshi la Uganda na Mkufunzi Mtendaji wa zoezi la ACIRC  FRANCIS OKELLO amesema itakuwa hatua ya muda mfupi ya kusaidia matatizo ya Africa kabla ya jeshi  maalum la Umoja huo.

 

Comments are closed.