AU YALAANI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SUDANI KUSINI

AU YALAANI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SUDANI KUSINI

Like
184
0
Thursday, 29 October 2015
Global News

MUUNGANO wa Afrika umelilaumu Jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.

Uchunguzi wa AU umebaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda Rais.

Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.

Comments are closed.