AU YATANGAZA KUTUMA WALINDA AMANI BURUNDI

AU YATANGAZA KUTUMA WALINDA AMANI BURUNDI

Like
254
0
Friday, 18 December 2015
Global News

MUUNGANO wa Afrika umetangaza mpango wa kutuma walinda amani nchini Burundi kuzuia machafuko zaidi nchini humo. Muungano huo umepanga kutuma walinda Amani elfu 5,000 wa kulinda raia.

 

Umoja wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili  baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.

 

AU huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji, muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu kuingilia kati katika mataifa mengine nyakati za hatari kubwa.

Comments are closed.