IMEELEZWA kuwa Mji muhimu wa mwisho uliokuwa mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU) -miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka usiku.
Majeshi kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.